Wednesday, February 13, 2013

RAIS JONATHAN AIMWAGIA SUPER EAGLES MAMILIONI.

RAIS wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza zawadi kwa ajili ya kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles katika sherehe maalumu ya kuipongeza timu hiyo kunyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika iliyofanyika jijini Abuja. Jonathan alitangaza kutoa kiasi cha naira milioni 10 kwa ajili ya kocha wa Super Eagles Stephen Keshi, naira milioni tano kwa kila mchezaji kwenye kikosi kizima cha wachezaji 23 na naira milioni mbili kwa viongozi wengine walioongozana na kikosi hicho. Pia rais huyo aliwagawia wachezaji wote wa timu hiyo kiwanja katika mji mkuu wan chi hiyo Abuja. Nigeria ilifanikiwa kunyakuwa kombe hilo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakati walipoifunga Burkina Faso katika mchezo wa fainali uliochezwa Jumapili iliyopita.

No comments:

Post a Comment