Monday, February 4, 2013
OBI MIKEL AJINYAKULIA KITITA CHA DOLA 5,000 KUTOKA KWA KALOU.
KIUNGO wa kimataifa wa Nigeria John Obi Mikel amejinyakulia cha dola 5,000 kutoka kwa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Salomon Kalou baada ya Nigeria kuiengua Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika jijini Rustenburg, Afrika Kusini. Nigeria ambao wanajulikana kama Super Eagles walifanikiwa kuwatoa Tembo wa Ivory Coast ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji la michuano hiyo kwa mabao 2-1. Kabla ya mchezo huyo Obi Mikel na Kalou waliekeana dau kila mmoja akidai timu yake itasonga mbele kwenye michuano hiyo lakini ilikuwa ni Kalou ambaye anacheza katika klabu ya Lille ya Ufaransa aliyelazimika kutimiza ahadi yake baada ya timu yake kutolewa. Akihojiwa Kalou mwenye umri wa miaka 27 aliwasifu wapinzani wao kwa kucheza mchezo mzuri na kwamba walistahili kushinda mchezo huo huku akidai kuwa ametimiza ahadi yake aliyompa Obi Mikel. Kwa upande mwingine Obi Mikel amesema juhudi za pamoja walizokuwanazo kwenye mchezo huo ndio siri ya ushindi wao waliopata dhidi ya timu hiyo ngumu. Nigeria sasa itakwaana na Mali katika mchezo wa nusu fainali itakayofanyika katika Uwanja wa Moses Mabhida uliopo jijini Durban Jumatano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment