Saturday, February 9, 2013

OLISEH EXPECTS KESHI TO PLAY MIND GAMES.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria-Super Eagles, Sunday Oliseh anategemea kocha wa sasa wa timu hiyo Stephen Keshi kutokuwa mkweli kuhusiana na hali za wachezaji wake nyota Victor Moses na Emmanuel Emenike ambao ni majeruhi. Wachezaji hao walipata majeraha wakati wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Mali ambapo Nigeria ilishinda kwa mabao 4-1 Jumatano iliyopita na sasa kumekuwa na wasiwasi kuwa nyota hao hawatacheza mchezo wa fainali dhidi ya Burkina Faso baadae leo. Oliseh ambaye amecheza michezo 63 ya kimataifa akiwa na Nigeria kati ya mwaka 1993 na 2001 alidai kuwa hategemea kocha huyo kutoa taarifa ya kueleweka kuhusiana na hali za Moses na Emenike. Moses anaelezewa kama mmoja wa wachezaji wa Nigeria mwenye maamuzi yanayofaa zaidi katika michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka huu wakati Emenike ni mojawapo ya wafungaji waliofunga mabao mengi zaidi akiwa na mabao manne.

No comments:

Post a Comment