Thursday, February 14, 2013
PISTORIUS AHOJIWA NA POLISI KUFUATIA MAUAJI YA MWANAMKE.
MWANARIADHA nyota mlemavu Oscar Pistorius anahojiwa na polisi kufuatia tuhuma za kumpiga risasi na kumuuwa mwanamke mmoja anayeaminika kuwa mpenzi wake nyumbani kwake jiji Pretoria, Afrika Kusini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na radio moja jijini Johannesburg imedai kuwa Pistorius alimpiga risasi mwanamke huyo kichwani na mguuni ingawa hata utata wa suala hilo haujawekwa wazi lakini inahisiwa alimuua mwanamke huyo kimakosa kwa kuhisi kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia. Bastola ndogo ya milimita tisa ilikutwa katika eneo la tukio na bado inafanyiwa uchunguzi huku mwanamke huyo akidai kupigwa risasi mara nne kabla ya kupoteza maisha. Polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa awali katika eneo la tukio na kuchukua maelezo kwa majirani wa eneo hilo huku Pistorius akitarajiwa kufikishwa mahakamani baadae leo. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki. Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment