Friday, February 8, 2013
RUNGU LA CAF LAMSHUKIA RENARD.
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limemtoza faini ya dola 10,000 kocha wa timu ya taifa ya Zambia, Herve Renard baada ya kocha kutoa kauli kwamba shirikisho hili lilifurahia timu yake kutolewa katika michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini. Zambia ambao walikuwa mabingwa watetezi katika michuano hiyo walitolewa katika hatua ya makundi baada ya kung’ang’aniwa sare ya bila ya kufungana na Burkina Faso ambapo Renard alidai kuwa CAF haikutaka timu yake ichukue kombe hilo kwa mara nyingine na kuiwakilisha Afrika katika michuano ya Kombe la Shirikisho nchini Brazil. Akihojiwa marabaada ya timu yake kuenguliwa kwenye michuano hiyo Januri 29 jijini Nelspruit Renard alilituhumu shirikisho hilo kwa kufurahia kuondolewa kwao kwasababu timu yake haina mvuto wa kwenda kushiriki michuano ya Shirikisho itakayofanyika baadae mwaka huu. Baadae kocha huyo aliomba radhi kwa maandishi na CAF walithibitisha kupata barua hiyo pamoja na Shirikisho la Soka la Zambia lakini pamoja na kumuonya bado wamemuwekea faini hiyo ili kuhakikisha hafanyi kitendo kama hicho siku za mbeleni. Zambia ambao ni mabingwa wa Afcon 2012 wamekosa nafasi ya kucheza michuano ya KOmbe la Shirikisho kwasababu CAF ilibadilisha michuano na kuiweka katika miaka isiyogawanyika na kulazimika kucheza kwa miaka miwili mfululizo yaani mwaka jana na mwaka huu. CAF tayari imeshathibitisha kuwa bingwa atakayepatika katika mchezo wa fainali utakaochezwa June kati ya Nigeria na Burkina Faso ndiye atakayepata nafasi ya kushiriki michuano ya Shirikisho itakayofanyika June.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment