Thursday, February 7, 2013
SITISHIKI KUFUNGWA NA UINGEREZA - SCOLARI.
KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe Scolari amesisitiza kuwa kufungwa kwa timu yake mabao 2-1 na Uingereza sio suala linalomkera sana ingawa aliwasifu wapinzani wake hao kwamba walistahili ushindi kwa kuonyesha kandanda la kiwango cha juu. Wayne Rooney alifunga bao la kuongoza kwa Uingereza baada ya Ronaldinho kukosa penati lakini bao hilo lilisawazishwa na Fred kwa kutumia vyema makosa yaliyofanywa na Gary Cahill huku bao la ushindi likifungwa na Frank Lampard aliyeingia akitokea benchi katika kipindi cha pili. Scolari amesema walikutana na timu nzuri yenye wachezaji imara waliokuwa katika kiwango bora hivyo hana sababu ya kusononeka kwa kufungwa kwani kuna baadhi ya vitu wamejifunza na sasa wanajua jinsi Uingereza wanavyocheza wanapokuwa katika kiwango bora. Kocha aliendelea kusema kuwa ameshazoea kupoteza mechi zake za kwanza pindi anapoanza kufundisha lakini baada ya mchezo wa kwanza anakuwa amezoea kushinda mechi zingine na mashindano kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment