Thursday, February 14, 2013
TANZANIA YAPOROMOKA TENA VIWANGO FIFA, NIGERIA YARUDISHA HESHIMA.
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry amesema ni vigumu kusikia mashabiki wakiwa tofauti na meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger wakati amebainisha anataka kurejea tena klabu hapo katika siku zijazo. Henry mwenye umri wa miaka 35 amesisitiza kuwa atu wanaomkosoa Wenger hawako sahihi kwa kufananisha ukame wa klabu hiyo kukosa vikombe kwa miaka nane haiondoi mafanikio aliyoipa klabu hiyo toka alipoanza kuifundisha. Medali ya mwisho kwa Arsenal kuvaa ilikuwa katika michuano ya Kombe la FA mwaka 2005 na wanakabiliwa na wakati mgumu wa kumaliza katika nafasi nne za juu ili waweze kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa hali ambayo imepelekea mashabiki wengi kuanza kupoteza imani na kocha huyo na kuanza kuhoji uwezo wake. Hatahivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Uingereza na mengine matatu ya Kombe la FA chini ya Wenger aliwaponda wanamkashifu kocha huyo kwa kuwakumbusha mafanikio waliyopata kipindi hicho. Henry amesema ni ngumu kusikia na kuona watu wanavyohoji uwezo wake katika kipindi hiki lakini ndio mchezo wa soka ulivyo wakati timu inapokosa ushindi mashabiki lazima watafute wa kumlaumu na siku zote kocha ndio huwa kimbilio lao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment