Monday, February 11, 2013
ZAMALEK KUCHEZA UWANJA MTUPU.
KLABU ya Zamalek ya Misri imetangaza kuwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya klabu ya Gazelle ya Chad utachezwa jijini Alexandria. Majeshi ya Misri yaliyopo jijini Alexandria mapema yalikataa kuhakikisha usalama kwa mechi za Ligi ya Mabingwa kwa timu za Al Ahly na Zamalek. Lakini Mkurugenzi wa Zamalek Alaa Mekled alibainisha kuwa majeshi ya usalama yaliyopo Alexandria sasa yamekubali kuhakikisha usalama wa mechi hiyo inayaotarajia kuchezwa katika Uwanja Borg Al Arab. Mekled amesema walizungumza na maofisa waliopo katika mji huo na kuwahakikishia kwamba watalinda hali ya usalama katika mchezo huo lakini utachezwa bila ya mashabiki lakini watajaribu kuzungumza nao tena kuona uwezekano wa kuwaruhusu baadhi ya mashabiki wachache ili waweze kuishangilia timu yao kwenye mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment