Thursday, March 14, 2013
AFRIKA ITANG'ARA KOMBE LA DUNIA 2014 - BECKENBAUER
NGULI wa soka wa Ujerumani, Franz Beckenbauer amesema timu za taifa za Afrika zinaweza kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 kutokana na mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa katika soka barani humo. Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 67 ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani Magharibi mwaka 1972 alitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za tuzo za michezo Duniani zilizofanyika jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Nguli huyo amedai mwaka 2006 wakati Kombe la Dunia lilipofanyika Ujerumani watu wengi walikuwa wakitegemea Ivory Coast itasonga mbele mpaka katika hatua ya nusu fainali lakini walishindwa na kutolewa katika hatua ya makundi. Ingawa lilikuwa suala la kukatisha tama lakini anaamini kuwa mwakni timu za Afrika zitafika mpaka katika hatua ya fainali kwa jinsi wachezaji wa nchi mbalimbali wanavyofanya vizuri ndani na nje ya Afrika. Mechi za kufuzu zinatarajiwa kuanza wiki ijayo kukiwa na timu 40 zitakazokuwa zikitafuta nafasi ya timu tano zitakazowakilisha bara la Afrika kwenye michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment