Thursday, March 14, 2013
FUFA YAIANGUKIA SERIKALI BAADA YA KUKABILIWA NA UKATA.
SHIRIKISHO la Soka nchini Uganda-FUFA wameiandikia barua serikai ya nchi hiyo wakiomba msaada wa kifedha ili ziwee kuisafirisha timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama The Cranes kwenda nchini Liberia. The Cranes inatakiwa kusafiri kuelekea jijini Monrovia wiki ijayo kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Liberia utakaochezwa Machi 24. Lakini FUFA hivi sasa ina madeni yaliyotakana na kuandaa michuano ya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-Cecafa na wanahitaji fedha kwa ajili ya kuihudumia timu hiyo. Ofisa habari wa FUFA Rogers Mulindwa alithibitisha shirikisho hilo kuzongwa na madeni hivi sasa lakini alikataa kuweka wazi kiasi gani walichoomba kwa serikali kwa ajili ya kuihudumia timu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment