Wednesday, March 13, 2013

AM BACK ON THE WHEEL - FERDINAND.

Rio Ferdinand akielekea mazoezini katika gari lake la kifahari.
BEKI wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand ameruhusiwa kuendesha gari tena baada ya kufungiwa kwa muda wa miezi sita kwa kosa kuendesha mwendo kasi mara tatu katika kipindi cha wiki tano. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ambaye anaweza kuitwa tena katika timu hiyo, aliwasili mazoezini akiwa gari lake aina ya Jaguar XJ ambalo alikamatwa nalo akiwa mwendo kasi mwaka uliopita. Mahakama ya Trafford ilikataa ombi la beki huyo akitaka asinyang’anywe leseni yake Septemba mwaka jana kwasababu anatakiwa kuwapeleka watoto wake wawili shule kila asubuhi.
Mara baada ya kumaliza adhabu yake Ferdinand aliandika ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter kuwa kitu cha kwanza alichofanya baada ya kuanza kuendesha gari tena ni kuwapeleka watoto wake shule.

No comments:

Post a Comment