Wednesday, March 13, 2013

YES WE CAN - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal amesema inabidi watumie uzoefu wao wote katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ili waweze kupindua matokeo ya mabao 3-1 waliyofungwa katika mchezo wa kwanza na kuifunga Bayern Munich katika mchezo wa pili utakaochezwa baadae leo. Wenyeji Bayern ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika mchezo huo wa pili utakaochezwa katika Uwanja wa Allianz Arena baada ya ushindi mnono waliopata katika Uwanja wa Emirates wiki tatu zilizopita. Kikosi cha Wenger kitajitupa uwanjani jijini Munich wakihitaji ushindi wa mabao matatu ili kuepuka kutolewa katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kwa miaka mitatu mfululizo. Arsenal itakuwa na kazi ngumu zaidi baada ya kuwakosa nyota wake tegemeo kama golikipa Wojciech Szczesny, kiungo tegemeo Jack Wilshere na beki Bacary Sagna. Wenger amesema mchezo utakuwa mgumu lakini anaamini ushindi kwa timu yake sio suala linashindikana.

No comments:

Post a Comment