QATAR YAJIPANGA KUANZISHA LIGI YA FEDHA NYINGI ZAIDI DUNIANI.
KLABU kubwa Duniani zimeripotiwa kutengewa fungu kubwa la fedha ili washiriki katika michuano itakayoshirikisha timu 24 nchini Qatar ambayo itakuwa ikichezwa kila baada ya miaka miwili. Gazeti la Times limeripoti kuwa familia ya kifalme ya Qatar inatarajia kutoa mpango wao mwezi ujao wa kutengeneza Dream Football League-DFL itakayoshirikisha klabu kama Manchester United na Barcelona ligi ambayo inaweza kutishia Ligi ya Mabingwa Ulaya. Qatar ambayo itaandaa michuano ya Kombe la Dunia 2022 wana malengo ya kuwa nguvu katika soka duniani na wameripotiwa kuwa tayari kutoa kitita paundi milioni 175 kwa kila klabu kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa michuano ya DFL inatarajiwa kufanyika kila baada ya miaka miwili kuanzia 2015 na itachezwa Qatar na kwenye majimbo mengine huko Ghuba.
No comments:
Post a Comment