Tuesday, March 12, 2013

ARSENAL INAHITAJI KUFANYA UWEKEZAJI WA KUTOSHA KAMA WANATAKA KUBAKIA KATIKA USHINDANI - ARTETA.

KIUNGO nyota wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta anaamini kuwa kunatakiwa kufanyika uwekezaji wa kutosha katika kipindi cha majira ya kiangazi kama klabu hiyo inataka kutafuta mataji tena msimu ujao. Baada ya timu hiyo kung’olewa katika Kombe la Ligi na Bradford City na lile la FA na Blackburn Rovers timu hiyo imekosa matumaini ya kunyakuwa taji lolote msimu huu ikiwa imepita miaka nane toka walipofanya hivyo mwaka 2005. Arteta anafikiri kuwa pengo kati ya vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester United na timu hiyo ni kubwa na kuonya kuwa bodi lazima igundue kuwa wanaporomoka kutoka katika ushindani kabla hawajachelewa. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa klabu hiyo ina msingi mzuri kuliko klabu yoyote ambayo amewahi kucheza na pia mfumo mzuri, wachezaji wazuri na fedha za kutosha ambazo wanaweza kufanya chochote hivyo haoni sababu kwanini klabu hiyo inasuasua badala ya kutumia nafasi hiyo kuwa kileleni. Wachezaji wengi nyota huvutiwa kwenda katika klabu ambayo watapata uhakika wa kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo hivyo Arteta anaamini kama Arsenal itakuwa ikishindwa kushika nafasi nne za juu ni wazi inaweza kuporomoka kiushindani kama ilivyokuwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment