Tuesday, March 12, 2013
INDIANA WELLS MASTERS: FEDERER, NADAL WATINGA 16 BORA.
WACHEZAJI nyota wa tenisi Roger Federer na Rafael Nadal wamejiweka katika nafasi nzuri ya kukwaana katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Indians Wells Masters baada ya wote kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora. Federer raia Switzerland anayeshika nafasi ya pili katika orodha za ubora duniani alifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumgaragaza Ivan Dodig wa Croatia kwa 6-3 6-1 katika mzunguko wa tatu ya michuano hiyo. Wakati Nadal yeye alifanikiwa kutinga hatua hiyo kirahisi zaidi baada ya mpinzani aliyetakiwa kucheza naye katika mzunguko wa tatu Leonardo Mayer kutoka Argentina kujitoa kutokana na maumivu ya mgongo. Federer ambaye ni bingwa mara nne wa michuano hiyo ya Indian Wells ilibidi apambane kudhibiti maumivu yake ya mgongo ili kushinda mchezo huo lakini amedai kuwa hadhani kama atapata tatizo hilo katika mchezo wake unaofuata dhdi ya Stanislas Wawrinka Jumatano. Kwa upande wa Nadal yeye atachuana na Ernests Gulbis wa Latvia katika kutafuta nafasi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment