Monday, March 11, 2013
BARCELONA YA SASA SIO KAMA YA ZAMANI - SACCHI.
KOCHA mkongwe Arrigo Sacchi anahisi klabu ya Barcelona watapata tabu kugeuza matokeo katika mchezo wao pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan kutokana na kuporomoka kwa kiwango cha timu hiyo. Sacchi ambaye amewahi kuinoa Milan anaamini kuwa Barcelona sio klabu bora kama ilivyokuwa katika misimu kadhaa iliyopita. Kocha huyo amesema timu hiyo sio ile iliyokuwa ikicheza katika kiwango cha juu kama ilivyozoeleka lakini tatizo hilo sio la kushangaza kwani mara zote huwezi kucheza kwa kiwango ambacho wengi wanategemea. Barcelona inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Milan katika Uwanja wa Camp Nou kesho baada ya kupoteza mchezo wa kwanza uliofanyika Italia kwa mabao 2-0. Sacchi amesema timu hiyo haiwezi kurejesha makali kwa siku moja au mbili ndio maana anaona mchezo wao marudiano utakuwa mgumu kwao baada ya kupoteza wa kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment