Monday, March 11, 2013
BAYERN HATARINI KUMKOSA RIBERY JUMATANO.
KLABU ya Bayern Munich inatarajiwa kumkosa mshambuliaji wake nyota Frank Ribery katika mchezo wao dhidi ya Arsenal utakachezwa Jumatano katika Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, Ujerumani. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliumia kifundo chake cha mguu wa kushoto katika mchezo wa Ligi Kuu nchini inayojulikana kama Bundesliga ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fortuna Dusseldorf mwishoni mwa wiki iliyopita. Mbali na nyota huyo Bayern pia itawakosa kiungo Bastian Schweinsteiger na beki Jerome Boateng ambao wote wamefungiwa mchezo mmoja huku winga Arjen Rubben akitarajiw akuanza baada ya kupona maumivu ya misuli yaliyokuwa yakimsumbua. Bayern itajitupa uwanjani ikiwa kifua mbele baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Emirates wiki tatu zilizopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment