Monday, March 11, 2013
USHINDI WA BARCELONA UTAONGEZA HAMASA KWENYE KIKOSI CHANGU - DEL BOSQUE.
KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque ana mategemeo kuwa Barcelona inaweza kubadilisha matokeo katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan ili kuongeza hamasa kwa kikosi chake kabla ya mchezo wao dhidi ya Ufaransa mwishoni mwa mwezi huu. Barcelona ilichabangwa mabao 2-0 na Milan katika mchezo wa kwanza uliochezwa San Siro lakini Del Bosque ambaye amewahi pia kuinoa Madrid amebaki na matumaini kwamba timu hiyo itakata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo katika mchezo wao wa marudiano utakaochezwa baadae usiku katika Uwanja wa Camp Nou. Kocha huyo amesema mchezo huo ni muhimu kwa Barcelona na Hispania kwani matokeo kama yakiwa mazuri itaongeza hamasa kwa wachezaji kaika timu ya taifa na kama wakipoteza kidogo wanaweza kukosa kujiamini. Kauli ya kocha huyo imekuja kutokana na wachezaji wengi nyota kutoka vilabu vya Barcelona na Real Madrid kuwa ndio wanaounda kikosi cha timu taifa ya Hispania ambayo inatarajiwa kuikaribisha Finland Machi 22 mwaka huu kabla ya kusafiri kwenda kucheza na Ufaransa siku nne mbele
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment