KIUNGO nyota wa zamani wa Uingereza, David Beckham ameteuliwa kuwa balozi wa kwanza wa kimataifa wa soka nchini China katika harakati za kusafisha taswira ya soka la nchi hiyo baada ya kukumbana na kashfa ya uapngaji matokeo na kukimbia kwa wachezaji nyota wa kimataifa katika Ligi Kuu ya nchi hiyo inayojulikana kama Super League. Kazi ya nyota huyo akiwa balozi itakuwa ni kuisaidia kwa kuiweka katika ramani ya dunia Super League pamoja na kukuza hadhi ya soka katika nchi hiyo. Beckham ambaye kwasasa anacheza soka katika klabu ya Paris Saint-Germain amesema amesema ana shauku na changamoto hiyo mpya aliyopata katika maisha yake ya soka na atafanya kila awezalo kuisaidia nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani.
Chama cha Soka cha nchi hiyo-CFA na kwa pamoja na wamefurahishwa na uteuzi huo ambapo wanaamini umaarufu wa nyota huyo utasaidia kuleta mabadiliko chanya katika soka lao.
No comments:
Post a Comment