Thursday, March 28, 2013

CAF YAIFUNGULIA LIBYA.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limeondoa adhabu ya kuifungia Libya kuandaa michuano ya soka. CAF iliifungia nchi hiyo iliyopo kaskazini mwa bara la Afrika kuandaa michuano ya Afcon kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoikumba nchi hiyo mwaka 2011. Timu ya taifa pamoja na klabu mbalimbali nchini humo zimekuwa zikicheza mechi zake za nyumbani katika nchi nyingine hususani Morocco, hata hivyo katika uamuzi mpya uliotolewa utaruhusu klabu ya Al-Nasr Benghazi kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho AS Far ya Morocco katika uwanja wa nyumbani mwezi ujao. Nchi ya Libya ilibadilishana miaka kwa kuiachia Afrika Kusini kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwaka 2013 na wao wataandaa michuano ya 2017. Waziri wa Michezo wan chi hiyo Abdessalem Ghouila amesema kuandaa michuano ya Afcon 2017 kutasaidia kuiridusha nchi hiyo katika hali ya kawaida baada ya vurugu za mapigano ambazo zilipelekea watu zaidi ya 25,000 kupoteza maisha.

No comments:

Post a Comment