Thursday, March 21, 2013

FERDINAND ATIMKIA QATAR.

Rio Ferdinand ambaye alijitoa katika kikosi cha Uingereza kitakacheza mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kutokana na matatizo ya mgongo yanayomsumbua, anatarajiwa kwenda nchini Qatar kufanya kazi ya uchambuzi katika luninga itakayorusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi ya Uingereza dhidi San Marino kesho. Beki huyo anayecheza klabu ya Manchester United amekubali kufanya kazi ya uchambuzi katika luninga ya Al Jazeera kwa ajili ya mchezo wa San Marino pamoja na kwamba itakuwa ni safari ya saa 15 mpaka makao makuu ya kituo hicho yaliyopo Doha. Ratiba hiyo ya safari itamsaidia nyota huyo kutatua tatizo lake la mgongo ambalo lilipelekea kujitoa katika kikosi cha Roy Hodgson. Mara baada ya kutua nchini Qatar mapema leo asubuhi Ferdinand aliandika katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa twitter kufurahia safari. Uamuzi wa mchezaji huyo kwenda Qatar unaweza kuwakera mashabiki wa soka wa Uingereza pamoja na Chama cha Soka cha nchi hiyo FA.

No comments:

Post a Comment