Thursday, March 21, 2013

WILSHERE NI MUHIMU ZAIDI KATIKA TIMU YA WAKUBWA - PEARCE.

KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya Uingereza, Stuart Pearce amedai kuwa kiungo nyota wa Arsenal, Jack Wilshere ana umuhimu zaidi katika timu ya wakubwa kuliko ya vijana. Pearce alithibitisha kuwa Wilshere hatakuwepo katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Ulaya baadae mwaka huu lakini anategemea michuano hiyo itakuwa muhimu zaidi kwa Alex Oxlade-Chamberlain. Kulikuwa na tetesi kuwa Wilshere angejumuishwa katika kikosi cha vijana lakini tetesi zilikanushwa na Pearce ambaye akiri mchezaji huyo ni muhimu zaidi katika kikosi cha wakubwa ambacho kinanolewa na Roy Hodgson. Pearce anaamini kuwa timu ya wakubwa ya nchi hiyo inaweza kupata mafanikio katika michuano mbalimbali kama utamaduni kushinda utajengwa kwa timu za vijana pia kushinda mataji.

No comments:

Post a Comment