Saturday, March 2, 2013
FIFA YAIMWAGIA SIFA LEBANON.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeipongeza Lebanon kwa hatua walizochukua dhidi ya suala la upangaji matokeo na kuhitaji maelezo zaidi juu ya wachezaji na waamuzi waliofungiwa kwa tukio hilo. Chama cha Soka cha nchi hiyo kimewapa adhabu tofauti wachezaji 24 ikiwemo adhabu ya kifungo cha maisha kwa beki Ramez Dayoub na mshambuliaji Mahmoud El-Ali kufuatia tuhuma za matokeo katika mechi za nyumbani na kimataifa. Uchunguzi wa miezi miwili uliofanyika na kuwahusisha mashahidi wapatao 60 ulikuwa ukiongozwa na katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Asia Magharibi-WAFF, Fadi Zreiqat uligundua kuwa baadhi mechi za vilabu na kimataifa zilikuwa zimepangwa. Katika taarifa yake FIFA ilipongeza shirikisho hilo kwa hatua walizochukua huku ikiwataka kuwatumia taarifa zaidi ili ziweze kuwasilishwa katika kamati ya nidhamu kuangalia uwezekano wa kuongeza adhabu. Soka barani Asia limekuwa ilikikumbwa na matukio ya upangaji matokeo katika siku za karibuni ambapo nchi za Korea Kusini na China nazo zimekumbwa na matukio kama hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment