Saturday, March 2, 2013
PLATINI ATAKA KOMBE LA DUNIA 2022 LIFANYIKE KIPINDI CHA BARIDI.
RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amesema michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Qatar 2022 italazimika kufanyika katika kipindi cha baridi ili kuwalinda wachezaji na mashabiki na joto kali. Qatar ilipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwaka 2012 na inatarajiwa kufanyika katika kipindi cha kiangazi ambapo nyuzi joto hufikia kiasi cha sentigredi 40. Platini ambaye aliipigia kura Qatar ipewe nafasi ya kuandaa michuano hiyo amesema kwasababu ya joto kali nchini humo michuano hiyo itabidi ichezwe katika kipindi cha baridi ambacho huwa katika miezi ya Desemba na Januari. Platini ambaye pia aliipigia kura Urusi kupata nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2018 aliendelea kusema kuwa kucheza soka katika joto kali linalofikia nyuzi joto 40 ni suala lisilowezekana kwa wachezaji. Suala hilo limezua mjadala mkubwa katika soka wadau wakihoji kwamba itakuwa ni suala lisilowezekana kusimamisha ligi zote kwa ajili ya kucheza Kombe la Dunia katika kipindi cha Desemba na Januari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment