Saturday, March 30, 2013

FIFA YAIPA TOGO DOLA 850,000.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeitoa kiasi cha dola 850,000 kwa Shirikisho la Soka nchini Togo-TFF kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2013 na 2014. Wawakilishi kutoka FIFA na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF walitembelea taifa hilo lililopo magharibi mwa Afrika jana na kutangaza kutoa kiasi hicho katika mkutano na vyombo vya habari. Mkuu wa kitengo cha mpango wa maendeleo wa FIFA, Cyril Loisel amesema sehemu ya fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuboresha michuano ya ligi daraja la kwanza na pili nchini humo. Ujumbe huo wa FIFA na CAF pia ulizungumza na viongozi wa TFF kuangalia uwezekano wa kuanzisha ligi ya soka ya wanawake nchini humo ili kuinua soka lao.

No comments:

Post a Comment