Saturday, March 30, 2013

VILANOVA AANZA KIBARUA.

MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova anaweza kurejea katika benchi la ufundi wiki ijayo wakati timu yake itakapochuana na Paris Saint Germain katika mchezo wa kwanza war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mapema wiki hii Vilanova alirejea nchini Hispania bada ya kupatiwa matibabu ya kansa kwa miezi miwili jijini New York, Marekani. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 ambaye alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Pep Guardiola mwanzoni mwa msimu huu alirejea katika mazoezi ya klabu hiyo lakini alishauriwa kutosafiri na timu hiyo katika mchezo wa leo wa La Liga dhidi ya Celta Vigo. Kwa upande mwingine beki wa kimataifa wa Ufaransa na Barcelona, Eric Abidal ametajwa katika kikosi kitakachocheza na Celta Vigo baada ya kupita mwaka mmoja baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini lingine. Abidal mwenye umri wa miaka 33 alifanyiwa upasuaji huo mwaka jana baada ya uvimbe uliogundulika kwenye ini lake Machi 2011 kurejea tena.

No comments:

Post a Comment