Saturday, March 30, 2013

BOLT KUREJEA LONDON JULAI.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, Usain Bolt anaweza kuwepo katika michuano ya kudhimisha mwaka mmoja wa michuano ya olimpiki iliyofanyika London mwaja baada ya wakala wake kubainisha kuwa wamefanya mazungumzo yenye kutia matumaini. Mbali na michuano ya olimpiki, Bolt hajashiriki mbio zozote zilizofanyika nchini Uingereza toka mwaka 2009 kwasababu ya sheria zao za kodi ambayo ilikuwa ikimlazimu kuacha kiasi cha pesa katika mbio zozote atazoshiriki na kukatwa makato katika pesa zozote anazopata kutokana na mikataba mingine. Hatahivyo msamaha kwa ajili ya wanariadha wasio wazawa uliondolewa katika bajeti hivyo kuwepo kwa uwezekano mkubwa kwa Bolt kushiriki michuano hiyo ambayo inatarajiw akufanyika Julai 26 hadi 28 mwaka huu. Waandaaji wa michuano hiyo wanamatumaini Bolt atarejea tena Uingereza katika michuano hiyo ikiwa kama sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya michuano ya radha ya Dunia inayotarajiwa kufanyika jijini Moscow baadae mwaka huu. Bolt mwenye umri wa miaka 26 alinyakuwa medali tatu za dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka jana, akiweka rekodi ya olimpiki katika mbio za mita 100 na kusaidia wanariadha wenzake kuweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za kupokezana vijiti za mita 400.

No comments:

Post a Comment