Wednesday, March 27, 2013

HAYE KUMTAJA MPINZANI WAKE KESHO.

BINGWA wa zamani wa ngumi wa uzito wa juu, David Haye anatarajia kutangaza pambano lake la kwanza toka alipopigana mara ya mwisho Julai mwaka jana. Haye mwenye umri wa miaka 32 alimtandika Dereck Chisora mwaka uliopita katika pambano ambalo liliwekewa vikwazo na Mamlaka ya Ngumi nchini Luxembourg. Bodi ya Ngumi nchini Uingereza iliwanyang’anya leseni mabondia hayo kufuatia kufanya vurugu na kutaka kuzipiga kavu kavu jijini Munich, Ujerumani Februari mwaka uliopita. Mara kwa mara Haye amekuwa akionyesha nia ya kupigana na bingwa wa dunia wa WBC Vitali Klitschko ingawa hata hivyo bondia huyo amekuwa akimkwepa. Kaka yake Vitali, Wladimir bingwa wa mikanda ya IBF, WBO na WBA ambaye alimtandika Haye mwaka 2011 anatarajiwa kukutana na Francesco Pianeta Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment