Thursday, March 28, 2013

MIAMI HEAT YASHINDWA KUENDELEZA UBABE MBELE YA CHICAGO BULLS.

TIMU ya mpira wa kikapu ya Miami Heat imeshindwa kuweka rekodi ya kufikisha michezo 33 bila kupoteza baada ya kufungwa na Chicago Bulls katika mchezo wa Ligi Kuu ya mpira huo nchini Marekani maarufu kama NBA. Heat ambao wamecheza mechi 27 bila kupoteza, wameshindwa kufikia rekodi ya mechi 33 iliyowekwa na timu ya Los Angeles Lakers katika msimu wa mwaka 1971-1972. Nyota Heat LeBron James ambaye ndio mchezaji mwenye thamani zaidi wa NBA amesema hakuna aibu yoyote kwao kushindwa kufikia rekodi hiyo. Katika mchezo huo James ambaye alikuwapo katika kikosi cha Marekani kilichonyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki 2012 alifunga alama 32 lakini juhudi hizo hazikuweza kuinusuru timu yake kupokea kipigo cha vukapu 101-97 kutoka kwa Chicago.

No comments:

Post a Comment