Sunday, March 10, 2013
MICHEZO KUENDELEA KAMA KAWAIDA MISRI.
Makamu wa rais wa Chama cha Soka nchini Misri-EFA, Hassan Farid amebainisha kuwa shughuli za kimichezo zitaendelea kama kawaida nchini humo. Kauli hiyo inakuwa imeingiliana na ile aliyotoa msemaji wa EFA, Azmy Megahed ambaye alidai mapema Jumamosi kuwa bodi ya chama hicho itasimamisha shughuli zote za kimichezo nchini humo. Farid amesema kauli iliyotolewa na Megahed ni mawazo yake binafsi kwani shughuli za kimichezo zitaendelea kama kawaida kwa mechi zote zilizopangwa kuchezwa leo kuendelea kama zilivyopangwa. Mamia ya mashabiki walivamia makao makuu ya EFA na kuataka kuwasha moto ofisi hizo baada ya hukumu ya kifo kutolewa kwa mashabiki 21 waliokuwa vinara katika vurugu za Port Said ambazo zilisababisha vifo vya watu 74.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment