Saturday, March 30, 2013

MURRAY, FERRER KUCHUANA FAINALI SONY OPEN.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya wazi ya Sony baada ya kumfunga Richard Gasquet wa Ufaransa kwa 6-7 6-1 6-2. Katika mchezo huo Murray ilibidi apigane kufa na kupona baada ya kupoteza seti ya kwa Gasquet ambaye alionekana kuwa katika kiwangi kizuri katika mchezo huo. Fainali ya michuano hiyo ambayo inafanyika jijini Miami, Florida inatarajiwa kutimua vumbi kesho ambapo Murray atachuana na David Ferrer wa Hispania. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Murray amesema mpinzani wake alimpa wakati mgumu kwenye mchezo huo hususani katika seti ya kwanza lakini anashukuru alirekebisha makosa aliyofanya na kuhakikisha anaibuka mshindi kwenye mchezo huo.

No comments:

Post a Comment