Sunday, March 31, 2013

MESSI AWEKA REKODI NYINGINE.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amefanikiwa kufunga bao katika mechi 19 mfululizo za Ligi nchini Hispania na kuweka rekodi mpya kwa kuifunga kila timu walioyokutana nayo katika ligi hiyo msimu huu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Argentina alitengeneza bao la kwanza na kufunga la pili lakini Celta Vigo ambao wanapambana wasishuke daraja walifanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 88 na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Hilo linakuwa bao lake la 30 katika mechi 19 ambapo sasa amefikisha jumla ya mabao 43 katika mechi 29 walizocheza msimu huu na kubakisha mabao saba kufikia rekodi ya mabao 50 aliyoweka msimu uliopita huku kukiwa kumebakia mechi tisa. Messi ambaye kwa mara ya kwanza katika mchezo alikuwa nahodha amesema anashukuru kwakuwa amekuwa na bahati ya kufunga na kuisaidia timu na huwa hatilii maanani rekodi anazovunja cha muhimu ni timu yake kushinda.

No comments:

Post a Comment