Sunday, March 31, 2013

MISRI WATAWAZWA MABINGWA WAPYA WA MICHUANO YA U20 AFRIKA.

TIMU ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ya Misri jana wametawadhwa mabingwa wapya wa michuano ya Afrika kwa vijana wa umri huo baada ya kuifunga Ghana kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka sare kwa kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida. Vijana hao wa Misri ambao wanajulikana kama The Young Pharoahs yaani Mafarao Wadogo hili linakuwa taji lao la nne kwa michuano hiyo wakiizidi Ghana kwa taji moja baada ya ya kulinyakuwa mara tatu. Katika mchezo huo Misri ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya ya nne kwa njia ya penati baada ya Saleh Gomaa kuangushwa katika eneo la hatari lakini iliwachukua Ghana dakika tatu kurudisha bao hilo baada ya wao pia kupata penati iliyofungwa na Jeemiah Arkoful. Baada ya kufungwa mabao hayo timu zte ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini mpaka mpira unamalizika na kuongezwa dakika 30 hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake hivyo kupelekea kupigiana matuta.

No comments:

Post a Comment