Sunday, March 31, 2013

SERENA AWEKA REKODI MICHUANO YA SONY OPEN.

MCHEZA tenisi namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams amefanikiwa kushinda michuano ya wazi ya Sony baada ya kumfunga Maria Sharapova kwa 4-6 6-3 6-0 na kuweka rekodi ya kunyakuwa taji hilo mara sita. Williams ambaye amefikia rekodi ya nyota wa zamani wa tenisi Steffi Graf ambaye naye amewahi kunyakuwa michuano hiyo ya Miami mara sita. Williams ambaye ni raia wa Marekani amefanikiwa kushinda taji hilo mwaka 2002, 2003, 2004, 2007 na 2008 huku akimaliza katika nafasi ya pili mwaka 1999 na 2009. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema kushinda yaji hilo ni kitu ambacho hakukitegemea wakati mashindano hayo yanaanza lakini anashukuru amepambana mpaka kuhakikisha ananyakuwa taji hilo kwa mara ya sita.

No comments:

Post a Comment