Sunday, March 31, 2013

O'NEILL ATIMULIWA SUNGERLAND.

KLABU ya Sunderland ambayo iko kwenye hatari ya kushuka daraja imemtimua meneja wake Martin O’Neill kufuatiwa matokeo mabaya ambayo imekuwa ikipata timu hiyo. Sunderland ambao wanajulikana kwa jina maarufu la paka weusi wako alama moja juu ya msatari wa kushuka daraja huku wakiwa wamebakiwa na michezo saba baada ya kufungwa na Manchester United Jumamosi. Klabu hiyo imesema wameamua kuvunja mkataba na O’Neill na kumshukuru kocha huyo katika kipindi chote alichokuwepo hapo pia kumtakia kila la kheri huko aendapo. Pia klabu hiyo imedai itatangaza mbadala wa O’Neill katika chache zijazo. Kuondoka kwa O’Neill kunafikisha idadi ya mameneja watano wa Ligi Kuu nchini Uingereza waliopoteza vibarua vyao wengine wakiwa ni Roberto Di Matteo wa Chelsea, Mark Hughes wa Queens Park Rangers, Nigel Adkins wa Southmpton na Brian MarkDermott wa Reading.

No comments:

Post a Comment