Saturday, March 9, 2013

MWAMUZI ALIYEPATA KIPIGO LEBANON AAMUA KUSTAAFU.

MWAMUZI wa soka nchini Lebanon Bachir Awasa amefurahi kutoka hai baada ya kupigwa na wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi katika mchezo wa ligi daraja la pili mwishoni mwa wiki iliyopita lakini mwamuzi huyo ameamua kuachana na mambo soka. Awasa alipigwa na kukimbizwa kuzunguka uwanjani jijini Beirut baada ya kumuonyesha kadi nyekundu mchezaji wa klabu ya Al-Nahda Jumamosi katika mchezo dhidi ya timu ya Al-Salam Zgharta. Akizungumza na waandishi wa habari mwamuzi huyo amesema kutokana na hasira za wachezaji na maofisa walizokuwa nazo mara baada ya kutoa kadi nyekundu hakutegemea kutoka mzima hivyo anashukuru tukio hilo halikufikia huko. Chama cha Soka nchini humo tayari kimetoa adhabu kwa wachezaji 24 kutokana na tukio hilo ikiwemo kifungo cha kimichezo cha maisha kwa beki Ramez Dayoub na mshambuliaji Mahmoud El-Ali. 

No comments:

Post a Comment