Saturday, March 9, 2013

MASHABIKI 21 WAHUKUMIWA KIFO MISRI BAADA YA VURUGU ZA PORT SAID.

MAHAKAMA nchini Misri imewahukumu kifo mashabiki wa soka 21 waliokuwa vinara wa vurugu zilizotokea uwanjani huko jijini Port Said mwaka uliopita kesi ambayo ilizua mapigano makali katika mji huo uliopo katika mto wa Suez. Mauaji hayo yalitokea Februari mwaka jana mwishoni mwa mechi kati ya Al-Ahly ya jijini Cairo na wenyeji wa mji huo timu ya Al-Masry. Watazamaji walikanyakagana wakati wakijaribu kutoka uwanjani baada ya mashabiki wa Al-Masry kuvamia uwanjani na kuanza kupigana na wengine kurushwa nje ya uzio. Akitaja majina ya watuhumiwa 21 jaji amesema mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na hivyo kuwahukumu mashabiki hao kunyongwa hadi kufa. Mbali na hao mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine watano kifungo cha maisha jela kwa vurugu hizo huku wengine 28 kati ya mashabiki 73 waliofikishwa mahakamani hapo wamepewa vifungo vya muda mfupi.

No comments:

Post a Comment