MCHEZAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos anadhani kuwa mshambuliaji nyota wa nchi hiyo Neymar atang’ara kama akihamia katika klabu ya Barcelona ya Hispania. Carlos anaamini kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 anayecheza katika klabu ya Santos angefaa zaidi kucheza katika klabu hiyo katika sijazo. Beki huyo aliendelea kusema kuwa amezungumza na mchezaji huyo na kwa mawazo yake anatakiwa awe ameshaondoka Brazil na Barcelona wana nafasi kubwa ya kupata saini ya nyota huyo. Mkataba wa Neymar na klabu ya Santos unaishia katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment