Sunday, March 3, 2013
MWEKEZAJI KUTOKA MASHARIKI YA KATI ATAKA KUINUNUA ARSENAL.
M’BIA kutoka Mashariki ya Kati anajipanga kuweka zabuni ya kiasi cha paundi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuimiliki moja kwa moja klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza. Katika taarifa zilizochapishwa katika gazeti la Telegraph la nchi hiyo wawekezaji hao kutoka Mashariki ya Kati hawakutaka kujitambulisha kwanza mpaka mchakato huo utakapoanza rasmi. Taarifa katika gazeti hilo iliendelea kuelezea mipango ya wabia hao kuwa wataweka fungu la kutosha kwa ajili ya usajili ili kuigeuza klabu hiyo kubwa kuwa tishio barani Ulaya na Duniani kwa ujumla. Zabuni hiyo inatarajiwa kuweka wiki chache zijazo, wakiwa na nia ya kununua hisa zote za mmiliki wa sasa klabu hiyo Stan Kroenke kutoka Maekani ambaye anamiliki kampuni ya vifaa vya michezo. Pia wabia hao wamepanga kupunguza bei ya tiketi katika Uwanja wa Emirates na kuejesha heshima ya klabu hiyo waliokuwa nayo kipindi wanacheza katika uwanja wao wa kihistoria wa Highbury. Wawekezaji kutoka Mashariki ya kati wamekuwa wakimiminika kwa wingi barani Ulaya kuwekeza katika soka ambapo tayari klabu kama Manchester City inamilikiwa na mmoja wa wanafamilia ya kifalme ya Abu Dhabi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment