SHABIKI MMOJA AFA KATIKA VURUGU HUKO ARGENTINA.
MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 31 amekufa katika vurugu za mashabiki kabla ya mchezo wa ligi daraja la pili nchini Argentina ambao ulizikutanisha timu za Gimnasia na Nueva Chicago. Polisi katika mji wa La Plata walimtaja mtu huyo aliyefariki kuwa ni Julio Vizaci aliyepigwa risasi ya tumbo na kukimbizwa hospitali ya San Martin na kupoteza maisha akiwa huko. Wakati huohuo kijana mwingine mwenye umri wa miaka 11 anaendelea vizuri baada ya kujeruhiwa katika tukio hilohilo na amehamishiwa katika hospitali ya Sor Maria Ludovica baada ya kupigwa risasi ya kiuno. Mashabiki waivamiana katika eneo la Pereyra Iraola kabla ya mchezo baina ya timu hizo ambapo Gimnasia iliifunga Chicago kwa mabao 4-0.
No comments:
Post a Comment