Sunday, March 3, 2013

NADAL ANYAKUWA TAJI LAKE LA PILI MEXICO.

MCHEZAJI tenisi nyota Rafael Nadal amefanikiwa kumfunga David Ferrer katika fainali ya michuano ya wazi ya Mexico na kushinda taji lake la pili toka arejee uwanjani baada kupona majeraha katika mguu wake wa kushoto. Nadal ambaye ni raia wa Hispania alikuwa akijiuguzi kwa kipindi cha miezi saba lakini sasa ameonekana kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida kwa kufanikiwa kushinda taji la pili katika kipindi cha wiki tatu baada ya kushinda pia taji la michuano ya wazi ya Brazil mwezi uliopita. Nadal mwenye umri wa miaka 26 alimfunga mhispania mwenzake Ferrer mwenye umri wa miaka 30 kwa 6-0 6-2 katika mchezo uliofanyika jijini Acapulco. Nyota huyo ambaye ameporomoka katika orodha za ubora duniani mpaka nafasi ya tano, aliishukuru familia yake na madaktari ambao walikuwa wakimhudumia katika kipindi chote ambacho amekuwa majeruhi na kudai kwamba anajisikia vyema.

No comments:

Post a Comment