Monday, March 4, 2013

RENARD AWATAKA MAOFISA NA WACHEZAJI KUNG'AMUA VIPAJI KWA USAHIHI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Zambia, Herve Renard amewataka wachezaji na maofisa wote wanaohusika na mpango ya kung’amua vipaji vya wachezaji kufanya kazi hiyo kwa usahihi muda wote. Renard alitoa kauli hiyo baada ya kumalizika kwa kipindi cha jana mchana na kusema wachezaji wote ambao watakuja kufanyiwa usaili wakiwa wamechelewa watakuwa moja kwa moja wamejiondoa kushiriki zoezi hilo. Kocha huyo amesema ili zoezi hilo lifanikiwe ni lazima kupata watu ambao wanaojali muda kwasababu kama kwenye usaili amechelewa hata ukimchagua ataendelea na tabia yake hiyo hivyo kushindwa kupata wachezaji sahihi wenye kujituma. Benchi la ufundi la timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na Renard wako katika msako wa kutafuta vipaji nchi nzima kwa ajili kuimarisha kikosi cha timu hiyo ambayo ilishindwa kutetea taji lake la michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon Januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment