Monday, March 4, 2013

PARK ATEMWA KOREA KUSINI.

MSHAMBULIAJI nyota kimataifa wa Korea Kusini, Park Chu-Young ametemwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa nchi hiyo ambacho kitacheza mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Qatar baadae mwezi huu. Park mwenye umri wa miaka 27 ambaye anacheza klabu ya Celta Vigo ya Hispania kwa mkopo katika klabu ya Arsenal ya Uingereza ameshindwa kuonyesha cheche zake baada ya kutofunga bao lolote toka Novemba mwaka jana. Korea Kusini inashika nafasi ya pili katika kundi A ambalo linaongozwa na Uzbekistan na wataikaribisha Qatar Machi 26 katika mzunguko wa mwisho wa mechi za kufuzu michuano hiyo kwa upande wa bara la Asia. Kocha wa timu hiyo alitetea uamuzi wake wa kumuacha Park akidai kuwa ameteua kikosi chake kutokana na uwezo wa wachezaji na viwango vyao katika vilabu vyao. Park ambaye amecheza katika michuano ya Kombe la Dunia 2006 na 2010 amecheza misimu mitatu katika klabu ya AS Monaco ya Ufaransa kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment