Wednesday, March 20, 2013

TOURE MGUU NJE MGUU NDANI CITY.

KIUNGO nyota wa klabu ya Manchester City Yaya Toure huenda akaondoka klabuni hapo baada ya klabu hiyo kukaa kimya juu ya mazungumzo ya mkataba mpya. Mkataba wa kiungo huyo ambao unamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 220,000 kwa wiki unafikia kikomo 2015 lakini wakala wake anataka klabu hiyo kumpatia mkataba mpya ifikapo Jumamosi na kama wasipofanya hivyo ataanza mazungumzo na vilabu vingine. Toure mwenye umri wa miaka 29 ameripotiwa kujisikia haitajiki klabuni hapo kutokana na klabu hiyo kushindwa kufanya mazungumzo juu ya mkataba mpya katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Wakala huyo Dimitri Seluk hadhani kama nyota huyo atabakia klabuni hapo lakini kama atasaini mkataba mpya ndani ya siku nne zijazo anaweza kubakia.

No comments:

Post a Comment