Wednesday, March 20, 2013

FA KUMPA UBALOZI OWEN.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kipo katika mazungumzo juu ya uwezekano wa mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa nchi hiyo Michael Owen kuwa balozi wa heshima wa chama hicho. Owen ambaye anacheza katika klabu ya Stoke City alitangaza kustaafu soka la kulipwa mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu kwa kipindi cha miaka zaidi ya 16. Lakini Mkurugenzi Mtendaji wa FA Adrian Bevington alibainisha kuwa chama hicho kina nia ya kuendelea kufanya kazi na Owen mwenye umri wa miaka 33 ambaye aliifungia nchi hiyo mabao 40 katika mechi 89 alizocheza. Bevington amesema Owen siku zote amekuwa akijitolea kwa nguvu zake zote wakati akiwa katika majukumu na timu ya taifa ya Uingereza kwa kucheza kwa kiwango cha juu na kufunga mabao muhimu katika michuano mikubwa. Hivyo wanadhani kwa uzoefu wake alioupata katika kipindi alichocheza soka anaweza kuutumia kwa wachezaji wanaochipukia wa nchi hiyo akiwa kama balozi.

No comments:

Post a Comment