SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limetangaza ratiba ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika shughuli iliyofanyika katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Nyon, Switzerland. Katika ratiba hiyo timu nane zitachuana kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali ambapo klabu tajiri ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa wenyewe wamepangiwa kucheza na Barcelona ya Hispania. Washindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita Bayern Munich ya Ujerumani wao watakuwa katika kibarua kizito baada ya kupangwa kucheza na vinara wa Ligi Kuu nchini Italia timu ya Juventus. Barcelona ambao ni mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2011 walitinga hatua hiyo baada ya kufanikiwa kugeuza matokeo ya mabao 2-0 ambapo timu nane zilizovuka hatua hiyo zitachuana baadae mwezi huu. Mabingwa watetetzi wa Ligi Kuu nchini Hispania Real Madrid watakwaanza na mabingwa wa soka nchini Uturuki timu ya Galatasaray wakati Malaga ya Hispania wao watakuwa na kibarua kizito kwa Borussia Dortmund ya Ujerumani. Mechi nne za kwanza zinatarajiwa kuchezwa baadae mwezi huu wakati mechi za marudiano zimepangwa kufanyika April 9 na 10. Ratiba ya nusu fainali inatarajiwa kupangwa April 12 huku fainali imepangwa kufanyika Mei 25 katika Uwanja wa Wembley nchini Uingereza.
EUROPA LEAGUE DRAW:
Chelsea v Rubin Kazan
Tottenham Hotspur v Basel
Fenerbahce v Lazio
Benfica v Newcastle United

No comments:
Post a Comment