Friday, March 15, 2013
INDIAN WELLS TOURNAMENT: NADAL AMTANDIKA HASIMU WAKE FEDERER NA KUTINGA NUSU FAINALI.
MCHEZAJI tenisi nyota Rafael Nadal amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya BNP Paribas kwa kumfunga hasimu wake Roger Federer wa Switzerland kwa 6-4 6-2 katika mchezo uliofanyika huko Indian Wells, California nchini Marekani. Katika mchezo huo Nadal ambaye ni raia wa Hispania alionyesha kiwango cha juu toka arejee baada ya kukaa nje kwa kipindi cha miezi saba kutokana na majeraha. Nadal ambaye anashika namba tano katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani sasa atakutana na Tomas Berdych wa Jamhuri ya Czech ambaye alimtoa Kevin Anderson wa Afrika Kusini kwa 6-4 6-4 katika mchezo war obo fainali. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Nadal amesema anajisikia furaha kutinga hatua hiyo baada ya kupita katika kipindi kigumu wakati akiwa majeruhi kwa miezi saba. Nyota huyo amesema alicheza vyema katika seti ya kwanza lakini katika seti ya pili hadhani kama mpinzani wake Federer alicheza katika kiwango chake cha kawaida kutokana na kustua maumivu yake ya mgongo ambayo yamekuwa yakimsumbua toka kuanza kwa michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment