Friday, March 15, 2013

VILLAS-BOAS AITAKA UEFA KUCHUKUA HATUA.

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspurs Andres Villas-Boas amelitaka Shirikisho la Soka Barani Ulaya-UEFA kuchukua hatua dhidi ya klabu ya Inter Milan baada ya kudai mshambuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor alifanyiwa vitendo vya kibaguzi katika mchezo wa Europa League baina ya timu hizo uliochezwa jana usiku. Adebayor alifunga bao muhimu katika dakika za nyongeza za mchezo huo ambazo ziliiwezesha timu yake kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo pamoja na kufungwa mabao 4-1 na Inter kwenye mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa San Siro. Kocha huyo amedai kuwa alikuwa akiwasikia mashabiki wa Inter wakipiga kelele za nyani kumlenga Adebayor. Wiki tatu zilizopita Inter walipigwa faini na kupewa onyo kuhusu mustakabali wa mashabiki wao katika siku za mbele kwasababu ya tukio kama hilo katika mchezo dhidi ya mahasimu wao AC Milan.

No comments:

Post a Comment