Friday, March 15, 2013
LANGALANGA: MASHINDANO YA ASTRALIA GRAND PRIX YASHIKA KASI.
DEREVA nyota wa mashindano ya langalanga kutoka timu ya Red Bull, Sebastian Vettel amemaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za majaribio kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano ya Australia Grand Prix. Vettel ambaye ni bingwa wa dunia alimzidi Felipe Massa wa timu ya Ferrari aliyeshika nafasi ya pili kwa sekunde 0.078 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Fernando Alonso ambaye naye anatoka timu ya Ferrari. Nafasi ya nne ilikwenda kwa Lewis Hamilton wa Marcedes na nafasi tano ilichukuliwa na Mark Webber wa Red Bull ambaye alimaliza mbele ya Kimi Raikkonen wa Lotus aliyemaliza katika nafasi ya sita. Kwa matokeo hayo timu nne ambazo ni Red Bull, Ferrari, Marcedes na Lotus ndio pekee zitakazoingia katika kinyang’anyiro cha kugombea kuanza mashindano hayo katika nafasi ya kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment