Friday, March 15, 2013
COLE NA FERDINAND WANATAKIWA KUSAHAU TOFAUTI ZAO KWA MASLAHI YA TAIFA - HODGSON.
KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amewataka Rio Ferdinand na Ashley Cole kumaliza tofauti zao kwa maslahi ya kikosi cha timu hiyo ambacho kinakabiliwa na michezo miwili ya kufuzu Kombe la Dunia 2014 dhidi ya San Marino na Montenegro. Wawili hao waliripotiwa kukwaruzana baada ya John Terry kushitakiwa kwa kumfanyia vitendo vya kibaguzi ndugu yake Ferdinand aitwaye Anton ambapo Cole alimtetea Terry mahakamani kitendo ambacho kilizua bifu kati yao. Lakini Hodgson amewataka nyota hao kuweka tofauti zao pembeni kwa maslahi ya timu ya taifa wakati watakapokutana tena. Hodgson amesema anajua wawili hao walikuwa marafiki na haoni kama tofauti walizonazo zinaweza kuwaathiri mpaka wakashindwa kutimiza majukumu yao kwani ni wachezaji waliopevuka na wanajua wanachokifanya pindi wawapo uwanjani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment